IRINGA: Basi la Abood lililokuwa likitokea Iringa kwenda Dar es Salaam limeligonga kwa nyuma basi la Happy Nation lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam kwenye milima ya Kitonga ambapo basi hilo liligonga lori la mizigo aina ya Fuso.
Katika tukio hilo mabasi hayo mawili yalitumbukia kwenye korongo lakini taarifa ya kifo au majeruhi bado hazijapatikana.
0 Comments