Tuma na kutoa pesa bure kupitia huduma ya Airtel money
· Wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure
· hakuna makato yoyote kwenye huduma ya Airtel money – “Hakatwi Mtu Hapa”
Dar es Salaam, Tanzania, Alhamisi 1st Agosti 2013
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa huduma za mawasilino leo imezindua ofa kabambe kwa watumiaji wa huduma ya kifedha ijulikanayo kama ‘Hakatwi mtu hapa’ inayowawezesha wateja wake nchi nzima kutuma na kutoa pesa kupitia huduma ya Airtel money bila makato yoyote.
Promosheni ya Airtel money Bure itatoa unafuu wa kiuchumi kwa wateja wengi wanaotumia huduma ya Airtel money.
akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando alisema “Airtel inaongoza kwa huduma bora zenye gharama nafuu nchini, na tunaendelea kutoa huduma zenye ubunifu kwa kuzindua promosheni mbalimbali kwa mwaka mzima.’Hakatwi mtu hapa’ promosheni tunayozindua leo ni mfano na mwendelezo wa dhamira yetu ya kufanya huduma ya Airtel money kuwa suluhisho na huduma bora ya kifedha nchi nzima”.
Kwa upande wake Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa aliongeza kwa kusema “ promosheni hii itawawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma na kutoa pesa kwenye mtandao wowote bila makato.
“Tunayofuraha kuweza kutoa unafuu kwa wateja kufanya miamala ya pesa bila makato yoyote na kuwaondolea gharama za kutuma na kutoa fedha zillizokuwepo hapo awali. Tumeamua kufanya hivyo ili kuwawezesha wateja wetu kupata kiasi chote cha pesa zao bila makato yoyote” aliongeza Singano.
Airtel kwa sasa inaendesha promosheni maalumu kwa wateja wake ya Airtel yatosha. promosheni ya ‘Hakatwi mtu hapa’ ni msisitizo unaoonyesha Airtel yatosha ambapo huduma zote ikiwa ni pamoja na kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi, huduma za internet na sasa kwenye huduma ya Airtel money ambayo inakuwa promosheni kabambe , nafuu kuliko zote nchini. Huduma ya Airtel money sasa bila shaka Yatosha
0 Comments