MNYAMA SIMBA LEO AMEUNGURUMA MARA BAADA YA KUUTUMIA VYEMA UWANJA WAKE WA NYUMBANI CCM KIRUMBA MBELE YA TIMU YA TOTO AFRICA AMBAPO SIMBA WENYEJI WA MCHEZO HU WALISHINDA 2-1, PICHANI WAKILISAKAMA LANGO LA TOTO.
MCHEZO ULIKUWA WA KASI TENA WA KUVUTIA KWA PANDE ZOTE MBILI ULIMALIZIKA KWA 0-0 KIPINDI CHA KWANZA.
PATASHIKA LANGONI MWA SIMBA.
BENCHI LA UFUNDI SIMBA.
MAJERUHI SIMBA UHURU SULEIMAN AMBAYE ALIUMIA VIBAYA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI.
DK YA 7 KIPINDI CHA PILI RASHID GUMBO AIPATIA SIMBA GOLI LA KWANZA KUPITIA KONA YAKE ILIYOMBABATIZA KIPA WA TOTO WILBERT MWETA KATIKA KUOKOA AKAUTUMBUKIZA MPIRA NYAVUNI.
KOCHA MKUU WA TIMU YA TANZANIA TAIFA STARS JAN POULSEN ALISIFU UWANJA WA CCM KIRUMBA KUWA NA PEACH NZURI NA PIA KUZIPONGEZA TIMU ZOTE MBILI KWA KUONYESHA MCHEZO MZURI WA KUVUTIA, KUHUSU LABDA KATIKA MCHEZO HUO LABDA KAONA WACHEZAJI KUTOKA TOTO ALIOPANGA KUWAITA STARS, KOCHA HUYO ALISEMA WATANZANIA WASUBIRI WATAONA MATOKEO.
PICHANI KOCHA WA SIMBA AKITETA JAMBO NA MWANASPOTI SALEHE ALLY.
EMANUEL OKWI ALIIPATIA SIMBA BAO LA PILI. TOTO WAKIPATA BAO DK YA 42 KUPITIA HUSEIN SWED BAADA YA GONGA GONGA ZA UKWELI ZILIZOWAPA PRESHA MASHABIKI WA SIMBA. HADI MWISHO SIMBA ILISHINDA 2-1.
0 Comments