Tarehe 21/may/2012 Tanzania imeadhimisha miaka 16 tangu meli ya MV BUKOBA kuzama ndani ya ziwa Victoria na kusababisha taifa kupoteza raslimali watu wake ambapo zaidi ya watu ELFUMOJA wanatajwa kufa maji kwenye ajali hiyo wakazi mbalimbali wa kanda ya ziwa jana walijumuika pamoja katika makaburi maalum ya marehemu hao yaliyoko eneo la Igoma jijini Mwanza kwaajili ya Ibada.
Katika maadhimisho hayo mwanamitindo Flaviana Matata amekabidhi msaada wa maboya (life vests) 500 kwa Kampuni ya usafirishaji abiria na mizigo mkoani Mwanza ya Marine ili kuimarisha kitengo cha usalama majini ikiwa ni katika kuwaenzi watu zaidi ya ELFUMOJA waliokufa maji akiwemo marehemu mama yake mzazi.




0 Comments