Zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Serikali mkoani Mwanza, kuwahamisha katikati ya Jiji wafanyabiashara wadogo (Machinga), ifikapo Desemba 3 mwaka huu, akina mama wauza samaki na mamalishe mkoani hapa wameangua vilio wakiomba kutohamishwa maeneo yao ya biashara na kujipatia riziki.
Leo mgambo pamoja na baadhi ya polisi wameonekana kutanda katika eneo la barabara kuu ya biashara soko kuu la jijini Mwanza almaarufu kwa jina la Market Street wakizuia wafanyabiashara wadogo (wamachinga) kutandaza bidhaa zao kwaajili ya kufanya biashara hali ambayo imewaweka njia panda akina mama hao wasijue pa kukimbilia.
Mbele ya ofisi za mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula zilizoko karibu na ukumbi wa mikutano almaarufu 'Ghand Hall', akinamama kwa makundi wamemiminika na kuzagaa maeneo hayo wakihaha kumsaka mbunge huyo ambaye tangu kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 aliahidi kuwasaidia lakini hata hivyo waliambulia patupu, kwa mbunge huyo kuwa nje ya ofisi hizo.
Prisca Hamisi ni mfanyabiashara wa samaki hapa anawasilisha 'Kilio' chake kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwamba watendaji wake wameyageuka maagizo yake BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
"Sasa hivi hata wanaume zetu uchumi ni mgumu wengine hawana kazi tumeona yale maisha ya kuitwa mama wa nyumbani siyo mazuri tumeamka kuingia mitaani kukopa mikopo ili tufanye biashara lakini leo hii kupitia kauli mbiu ya 'Hapa Kazi Tu' tumeamua kweli kufanya kazi, lakini kutokana na hii kazi kusitishwa tutakula wapi, jeh tugeuke ombaomba, tuishi mazingira gani, watoto wetu watasoma vipi ile hali wengine maisha ya ujanja ujanja hatuawezi?" BOFYA PLAY KUSIKILIZA
aaaa
0 Comments