Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

MEYA WA JIJI LA MWANZA AWATUNUKU VYETI WANA UKWATA CHUO CHA MIPANGO MWANZA

Mgeni rasmi Meya wa jiji la Mwanza akihutubia kweye mahafali ya UKWATA kwa wahitimu wa Chuo cha Mipango Bwiru Mwanza.
Wahitimu.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini jijini Dar es salaam Godwin Gondwe ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha ITV akitoa neno kwa wahitimu wa UKWATA Chuoni hapo alipoambatana na Meya Mabula.
Sehemu ya wanachuo wanachama wa UKWATA waliohitimu wakati wakiwa kwenye sherehe yao ya kuagwa jana Bwiru.
Kwaya ya UKWATA wakitumbuiza kwenye sherehe hiyo.
Kwaya ya Vijana Bwiru AICT wakitumbuiza kwenye mahafali.
Kwaya ya Vijana Bwiru AICT wakitumbuiza kwenye mahafali.
Wadau wa UKWATA.
Shambulia..
Meza kuu.
Engo nyingine ya wadau wa UKWATA.
Keki zikitinga tukioni.
Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akikata keki kuashiria uzinduzi wa maafali hayo.
Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akimlisha kipande cha keki mmoja kati ya wanakwaya wa Vijana Bwiru.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini jijini Dar es salaam Godwin Gondwe ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha ITV akimlisha keki mmoja kati ya wahitimu wa UKWATA Chuo cha Mipango Mwanza.





Na PETER FABIAN,
MWANZA.

MEYA wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (CCM) amewataka wahitimu wa vyuo vikuu nchini  wasiwe na mtizamo pekee wa kuajiriwa bali wawe na dhana ya ujasiriamali.

Mabula ambaye ni Diwani wa Kata ya Mkolani, aliyasema hayo jana akiwa mgeni rasmi kwenye mahafari  ya kuwaaga vijana wa Umoja wa Kikiristo Wanafunzi Tanzania(UKWATA) wahitmu katika  Chuo cha Mipango Mwanza .

“ hivi sasa  matarajio makubwa ya vijana mnaohitmu katika vyuo vikuu mbalimbali nchini ni mnamtamo wa kuajiriwa na serikali lakini bado mnaowajibu wa kujifunza bila kuwazia ajira pekee za serikali na kufikiria zaidi fursa za ujasiriamali,” alisema.

Pia kuna baadhi ya wahitimu wamekuwa na mwelekeo wa kuingia katika ulingo wa siasa lakini ulimwengu wa kisasa kataika  siasa ni tofauti na siku za nyuma hivyo wasomi mnapaswa kuwasaidia wenzenu wasio waelewa ili kuendea kuhubiri  amani na upendo kujenga umoja wa utaifa wetu.

“ ni kweli taifa lina bomu ambalo ni ukosefu wa ajira kwa vijana hivyo ni vyema vijana mkajitambua na kutumia elimu yenu kuhakikisha mnasimamia na kuilinda misingi imara  iliyoaachwa na waasisi wa taifa hili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali kufikia malengo tuliyojiwekea,” alibainisha.

Awali wahitimu UKWATA wakisoma risala kwa mgeni rasmi Imani Magawa na Rahel Sendeu waliomba kusaidiwa vifaa vya muziki wa injili, vitambaa kwa ajili ya madhabahu ambavyo gharama yake ni kiasi cha milioni 5.2 ili kuwezesha kwaya ya UKWATA na Vijana Bwiru AICT kukamilisha tungo za nyimbo.

Naye  Mhadhiri wa Chuo Kikuu Tumaini cha jijini Dar es salaam Godwin Gondwe  ambaye alipata fursa ya kuwaasa vijana hao kutojiingiza katika siasa zenye mwelekeo wa kuwagawa watanzania na kulisambaratisha taifa badala yake wazingatie taaluma walizopata ili kuwajengea uwezo wa kuajiriwa mahala popote pia kujiajiri katika ujasiriamali.

Gondwe, maarufu kwa jina la dabo “G” ambaye pia ni mtangazaji wa kituo kimoja cha Luninga nchini alikubali kuchangia  gharama zitakazohitajika kwa vitambaa vya mapambo na madhabahu ambapo fedha zake atazitoa baada ya kuwasilishwa gharama zake.

Huku Meya Mabula akichangia kiasi cha Shilingi milioni moja  mbali ya kuwalisha keki wahitimu wote wa UKWATA kwa shilingi laki nne pia zikachangwa jumla ya shilingi laki sita nyingine kutoka kwa wahitimu na waalikwa.

Post a Comment

0 Comments