Maandamano ya wafuasi na wanachama wa CHADEMA wakimsindikiza "Aliyekuwa mbunge wao" wa Arusha mjini ndugu Godbless Jonathan Lema kuelekea viwanja vya Ngarenaro majira ya saa nane na dakika 15 ambapo hatimaye alihutubia wananchi. Mahakama imetengua ubunge wa Lema kutokana na kesi iliyofunguliwa na wanachama watatu wa CCM.
Godbless Jonathan Lema amekubali uamuzi wa mahakama na amesema haina haja ya kukata rufaa isipokuwa ATASHINDA TENA kiti hicho katika uchaguzi mdogo utakaoandaliwa na tume ya Taifa ya uchaguzi. PICHA/HABARI NA SUBI
0 Comments